|
“TUNAJUA shangazi anatutesa kwa sababu baba na mama wapo mbali, kama wangekuwepo hapa tusingeteswa hivi. Tunamuomba baba, tunamuomba mama kama watasoma habari hii waje watuchukue turudi nyumbani, shangazi anatutesa sana, wala hatukutegemea,” ndivyo alivyoanza kusema mtoto Hassan Yusuf (5) ambaye ni mkubwa kwa wenzake, Hussein Yusuf (5) na Rehema Said (5). Ikifika mahali mtoto mdogo anasema anawakumbuka wazazi wake kwa sababu ya mateso anayoyapata ugenini ujue ni zaidi ya ukatili, tena ni ukatili wa kutisha. Watoto hao, kwa sasa wanaishi Nzasa ‘A’, Kata ya Charambe, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam na ndiko walikopatia mateso yote. MAMBO YALIPOANZA KUTIBUKA Wiki iliyopita, watoto hao waliokolewa na majirani katika kifungo cha miezi sita ndani huku afya zao zikiwa zimedhoofu kwa kukosa chakula. Ilidaiwa kwamba, watoto hao Hassan na Hussein ambao ni mapacha na Rehema, walifungiwa katika banda la shangazi yao aitwaye Asia Bora ambalo ujenzi wake haujakamilika. Wamekuwa wakiishi humo kwa kula mabaki ya vyakula jalalani. Watoto Hassan Yusuf, Hussein Yusuf na Rehema Said baada ya kuokolewa na majirani. USHUHUDA WA MAJIRANI Wakizungumza na gazeti hili hivi karibuni, majirani wa nyumba hiyo walimweleza mwandishi wetu kuwa watoto hao wamekuwa wakionekana nje ya nyumba hiyo mara chache sana wakiwa wanagombania mabaki ya vyakula kwenye jalala. “Tumekuwa tukiwaona nje mara chache kwenye jalala. Unajua, Asia (shangazi yao) aliwachukua kwa kaka yake, Kijiji cha Namakongoro Kata ya Lihimalyao huko Kilwa mkoani Lindi. “Tukasikia lengo lake aje kuishi nao kwa vile yeye Mungu hamkujalia kupata watoto. Lakini maisha hapo kwake yakawa siyo mazuri kwa kipato kwa mama huyo. Mmoja wa majirani hao aliyejitambulisha kwa jina la Aisha Ramadhan yeye alikwenda mbele zaidi kwa kusema: “Hapo awali tulikuwa tukiwaona wakitoka nje na kucheza na watoto wetu huku wakiwa na afya nzuri. Asia akatueleza kuwa ni watoto wa nduguye, amewachukua huko kijijini. “Baada ya muda fulani tukawa hatuwaoni, tulidhani amawarudisha kwao, lakini kadiri siku zilivyokuwa zinakwenda mbele tukawa tunawaona mara chache wakiwa jalalani wanapigania mabaki ya chakula. “Kuna siku mimi niliwakamata wakiwa wamebeba mfuko wa rambo wenye kinyesi, walikuwa wanakuja kutupa katika maeneo yetu, nikawarudisha nao kwa shangazi yao. Kumbe nyumba wanayoishi haina choo ndiyo maana wamekuwa wakijisaidia kwenye rambo. “Siku moja walipotoka nje kutafuta chakula jalalani, mimi na majirani wenzangu tuliwauliza wanaishije? Wakatuambia hawapewi chakula na shangazi yao akitoka asubuhi harudi mapema, akirudi inakuwa ni usiku sana wao wakiwa wameshalala. “Inasikitisha sana kuwaona watoto hawa wanaachwa peke yao kutwa nzima bila mtu wa kukaa nao na wamekuwa wakifungiwa ndani kwa muda mrefu sasa, ila huwa wanakiuka masharti na kutoka kwa ajili ya kutafuta mabaki ya chakula. Jirani huyo akaendelea kuanika mateso ya watoto hao: “Kwa kuwaonea huruma tumekuwa tukilazimika kuwapa chakula, lakini Asia anaporudi na kugundua hilo anawapiga, kwa hiyo wakawa waoga kuja kuchukua chakula. Mimi niliumia hadi machozi.” Jirani: “Baadaye wakawa hawaonekani, lakini cha ajabu mara nyingi tukiamka asubuhi tunakuta mifuko ya rambo yenye vinyesi imetapakaa, tukimweleza Asia inakuwa ugomvi. “Siku moja baada ya shangazi yao kuondoka, nilikwenda kuwachungulia ndani, nikawaona wamekonda sana, wamepauka na wamevaa nguo zilizochakaa. “Nilitokwa machozi, nililazimika kuwaita wenzangu nao walipofika hakuna aliyejizuia kulia. Tukasema hawa watoto watakufa, ndiyo tukaamua kuwaokoa kwa kupeleka taarifa kwa mzee Dadi Salum ambaye ni polisi jamii wa hapa. POLISI JAMII NAYE ALIA “Mzee Dadi naye alipofika na kuwaona kwa macho alilia, watu wakaanza kukusanyika, tukawatoa nje watoto, kila mmoja aliwaonea huruma. Tuliwachukua hadi Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Nzasa A. SHANGAZI MTU ANUSURUKA KIPIGO “Hatujui ni nani aliyempigia simu Asia, kwani muda mfupi tu tukasikia yupo nyumbani kwake. Uongozi wa mtaa ulimfuata, walipofika, wanawake wenzake hasa wale anaochukua nao mkopo wa fedha benki walitaka kumpiga wakimuuliza pesa anapeleka wapi. “Hata hivyo aliokolewa na polisi jamii ambao walimchukua na kumweka katika Bajaj na kumpeleka Kituo cha Polisi Mbagala kwenye Dawati la Jinsia na Watoto, watoto nao pia walipelekwa huko.” Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nzasa A, Mrisho Salum alikiri kuwapokea watoto hao wakiwa katika hali mbaya kiafya, wakapelekwa polisi. Akawataka wananchi kutokaa kimya mara wanapoona vitendo kama hivyo. Mwandishi alifika hadi kituo cha polisi na kuambiwa na askari mmoja kuwa mapacha walichukuliwa na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Othman Mbwana aliyedai ni babu yao. Mbwana alidai kwamba ameamua kuwachukua watoto hao wakaishi nyumbani kwake wakati akifanya mawasiliano na wazazi wao. “Kwanza nitawapeleka hospitali wakatazamwe afya zao, ila nimesikitishwa sana na hali hii, sijajua ni kwa nini watoto hawa wamefikia hatua hii,” alisema Mbwana. Rehema yeye alichukuliwa na mjomba wake aitwaye Sood Ismail ambaye alidai anakwenda kukaa naye hadi hapo atakapofanya mawasiliano na wazazi wa huyo mtoto, akisema kitendo cha Asia kimeidhalilisha familia.
RPC KIONDO
>>Bofya Hapa Kulike Page Yetu Kwa Story Zaidi za Kusisimua>> |
Tafuta katika Blogu Hii
Jumanne, 31 Desemba 2013
UNYAMA WAKUTISHA WATOTO DAR WAFUNGIWA NDANI MIEZI 6 NA MATESO MENGI TIZAMA HAPA
Jumatano, 11 Desemba 2013
SOMA MANENO MATAMU YA MANDELA ALIYOKUWA AKIMUANDIKIA KWA BARUA WINNIE WAKATI YUPO GEREZANI.
From a letter dated Oct. 26, 1976:
My dearest Winnie,
I
have been fairly successful in putting on a mask behind which I have
pined for the family, alone, never rushing for the post when it comes
until somebody calls out my name. I also never linger after visits
although sometimes the urge to do so becomes quite terrible. I am
struggling to suppress my emotions as I write this letter.I have received only one letter since you were detained, that one dated August 22. I do not know anything about family affairs, such as payment of rent, telephone bills, care of children and their expenses, whether you will get a job when released. As long as I don't hear from you, I will remain worried and dry like a desert.
I recall the Karoo I crossed on several occasions. I saw the desert again in Botswana on my way to and from Africa--endless pits of sand and not a drop of water. I have not had a letter from you. I feel dry like a desert.
Letters from you and the family are like the arrival of summer rains and spring that liven my life and make it enjoyable.
Whenever I write you, I feel that inside physical warmth, that makes me forget all my problems. I become full of love.
ANOTHER LETTERS
| These are just a few of the letters Mandela wrote from Robben Island where he was sent in 1964 at the age of 46. Eighteen of his 27 years in prison were spent on the prison island. | |
| April 15, 1976 My dearest Winnie, Your beautiful photo still stands about two feet above my left shoulder as I write this note. I dust it carefully every morning, for to do so gives me the pleasant feeling that I'm caressing you as in the old days. I even touch your nose with mine to recapture the electric current that used to flush through my blood whenever I did so. Nolitha stands on the table directly opposite me. How can my spirits ever be down when I enjoy the fond | |
Jumanne, 10 Desemba 2013
Kisa cha jamaa aliye muoa mwanamke asiye binadamu wa kawaida.
Kisa cha jamaa aliye muoa mwanamke asiye binadamu wa kawaida.
Jamaa mmoja alitoka Mbeya na kwenda Tanga kutafuta maisha, kufika kule akapata bahati ya kuwa meneja katika kiwanda kimoja maarufu pale jijini.Kijana huyu alikuwa ni mtu wa kujirusha sana na alikuwa akiamini ya kuwa hakuna furaha zaidi ya kula bata akiwa bado mzima na meno yangali yapo.
Siku moja akiwa club majira ya usiku akakutana na demu mmoja wa ukweli sana (chotara) na kucheza nae huku akimtupia maneno jamii ya ndoano ili aweze kumnasa yule manzi.
Muda wa kuondoka wakaondoka wote na kwa kuwa anakaa karibu na ule ukumbi hakuchukua cab akatembea uchochoroni na kufika home na kisha akajisevia ule mzigo.
Asubuhi akashangaa kuamka na kushuhudia yule manzi hayupo pale akaenda bafuni na sehemu zote akaona hakuna dalili ya yule binti basi akaamua alale zake hasa ukizingatia ilikuwa ni mapumziko ya kusherehekea siku ya uhuru.
Zikapita siku kadha siku moja akiwa anarudi home majira ya saa nne usiku akakutana na yule dada uchochoroni na kumwambia kuwa alikuwa anamsubiria jamaa, na chakushangaza kabisa yule binti akamwita jamaa kwa jina halisi wakati yeye alimtajia jina feki kama haya tuyatumiayo hapa facebook.
Wakaongea pale na jamaa akamvutia home na mambo yakaendelea kama kawaida yao na baada ya kukaa kwa muda mrefu jamaa akamwomba demu aende kuwaona wazazi wake na kujitambulisha ili wajue wana mkwe wao mtarajiwa.
Baada ya mvutano wa siku kadha demu akiwa anakataa hatimaye akakubali waende zao na kumwahidi atamfuta siku ya pili na wakutane hotel moja karibu na ufukwe wa bahari ya hindi.Jamaa akauliza sasa kwa nini twende jioni si tutachelewa kwani ni wapi?
Demu akamwambia usijali kabisa yaani.
Siku ya pili jioni jamaa akafika pale hotelini wakakaa karibu na ufukwe wakipiga story na kisha giza lilipotanda akamchukua jamaa na wakawa wanaifuata bahari na walipoanza kugusa maji binti akamwambia jamaa apande mgongoni mwake na afunge macho asifungue mpaka atakapo mwambia afumbue.
Baada ya kumbwambia afumbue wakawa wako kwenye mji mmoja wenye watu weupe jamii ya watu wenye asili ya bara Asia na kuna mtu akaja naongea kiswahili bomba na kuwaambia wavue zile nguo walizotoka nazo duniani na kupewa nguo za hariri ambazo ndio zavaliwa huko.
Baaada ya kuvaa akapewa chumba na muda mfupi baadae akaitwa na wazazi ambao wao wakaanza kumsimulia jamaa maisha yake kutoka akiwa mbeya mpaka pale tanga na kumwambia kwamba wamekubali amwoe mtoto wao ila kwa masharti ya kutofanya kazi na kuishi nae kwani hela wao watawapa.
Akwa anashangaa anataka kujua hizo hela zitakuwa na malipo? basi baba akamwambia kijana mmoja ampeleke store yule mkwe na kumwonyesha fedha za mataifa mbalimbali zikiwa kwenye kile chumba.
Basi jamaa akakaa pale kwa siku tatu, ile siku ya mwisho akaambiwa sasa atarudi kazini, ingawa ametafutwa kwa muda na bosi bila kuonekana atapewa barua ya kuachiswa kazi yeye aichukue bila hofu na baada ya siku ya tatu ataitwa arudi kazini na kuongezewa marupu rupu ila yeye akatae.
Basi kijana siku ya pili asubuhi akajikuta yuko home kitandani na wakati anafikiri anaota yule binti kaja na kusema yeye anarudi kwa wazazi hivyo atakaa kidogo kule kisha atarudi tena baada ya siku kadha na kumwambia jiandae usije chelewa kazini.
Kijana akaenda kazini na kupata barua ya kuachishwa kazi na siku ya tatu akaitwa na kagoma na yule binti akawa sasa karudi. Wakakaa mwaka mmoja na kuzaa mtoto mmoja na kisha kijana akamwambia anataka x-mass waende mbeya wakasalimie.
Wakati wako kwenye basi kwenda mbeya kila wakikaribia sehemu ya kupata chakula binti anatoweka kwenye gari na wakikaribia kituoni binti basi likisimama anakuja akiwa na chakula tayari.
Jamaa akawa anashangaa ila hana cha kuuliza, walipofika mbeya binti akagoma kabisa kuonana na wazazi wazazi wa yule kaka akitaka abaki hotelini na baada ya kulazimishwa mama yeye akasema lazima tumwone aliyekuzalia mtoto bomba kama huyu.
baada ya mama kuja na kumwona yule binti siku ya pili yake akafa huku binti akigaramia kila kitu na baada ya msiba kwisha wakarudi tanga na wakiwa njiani wakapata ajali ya basi kaka na mtoto wakapona ila dada yule mpaka leo hajulikani kama alitowekaje maana mpaka sasa ni mwaka wa saba hajatokea na wala hakuna dalili na mtoto yule sasa yupo darasa la kwanza na kaka anaogopa kuoa kwani hajui nini kitatokea binti akirudi kama kawaida yake bila taarifa.
HII NDO KAULI YA MWISHO YA WEMA KUHUSU DIAMOND
"SIWEZI KUSHINDANA NA DIAMOND KWASABABU MIMI SIO MWIMBAJI"...WEMA.

Je wewe ni kati ya wanaoamini kuwa wapenzi ‘wa zamani’ Wema Sepetu na Diamond Platnumz wanashindana kwa namna yoyote? Star wa kipindi cha ‘In My Shoes’ Wema Sepetu ameshare ujumbe kwa wote wanaofikiria hivyo.
Kupitia Instagram ameandika kuwa kitu pekee kinachosababisha watu wahisi hivyo ni kutokana na wote wawili kuwa na mafanikio katika fani zao (muziki na movie), na kuongeza kuwa hawezi kushindana na Diamond sababu yeye sio muimbaji.
MANJI ABWAGA MANYANGA YANGA, AWATEUA SEIF MAGARI NA BENNO VILLA KUWA VIONGOZI WAPYA JANGWANI
MANJI ABWAGA MANYANGA YANGA, AWATEUA SEIF MAGARI NA BENNO VILLA KUWA VIONGOZI WAPYA JANGWANI
Na Mwandishi Wetu, Jangwani
MWENYEKITI wa klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam, Yussuf Mehboob Manji amesema hatagombea tena nafasi hiyo baada ya kumaliza muda wake Julai mwakani.
Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Kariakoo, Dar es Salaam, Manji amesema ameamua mwenyewe kutogombea bila shinikizo na kikubwa amefuata demokrasia.
“Nina
miezi saba kabla ya uchanguzi mkuu mwakani, hivyo sasa ninajitahidi
kukamlisha shughuli zote ambazo nilianza kuzifanya ndani ya Yanga nikiwa
kama Mwenyekiti ili uongozi mpya utakaoingia uweze kuendeleza mipango
ya kuifanya Yanga iwe klabu bora Tanzania,”alisema.
Pamoja na hayo, Manji amemtambulisha Beno Njovu kuwa Katibu Mkuu mpya wa klabu, akichukua nafasi ya Lawrence Mwalusako aliyekua anakaimu kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa.
Manji amesema Beno Njovu anaanza kuitumikia hiyo nafasi mpya kuanzia leo na Mwalusako atakua naye pamoja kwa kipindi cha mwezi mmoja hadi atakapomkabidhi kazi rasmi.
Aidha, Manji amesema Mkutano Mkuu wa wanachama utafanyika Januari 19, mwakani na wanachama watapata fursa ya kupitia taarifa ya mapato na matumizi pamoja kujadili ajenda nyingine mbalimbali.
Pamoja na hayo, Kikao cha Kamati ya Utendaji kilichoketi mwishoni mwa wiki, kimemteua Seif Ahmed ‘Magari’ kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kimataifa na kutokana na nafasi hiyo pia ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Utendaji.
MWENYEKITI wa klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam, Yussuf Mehboob Manji amesema hatagombea tena nafasi hiyo baada ya kumaliza muda wake Julai mwakani.
Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Kariakoo, Dar es Salaam, Manji amesema ameamua mwenyewe kutogombea bila shinikizo na kikubwa amefuata demokrasia.
![]() |
| Manji kushoto, akizungumza na Waandishi wa Habari leo na kulia ni Beno Njovu katikati, Ofisa Habari wa klabu, Baraka Kizuguto |
Pamoja na hayo, Manji amemtambulisha Beno Njovu kuwa Katibu Mkuu mpya wa klabu, akichukua nafasi ya Lawrence Mwalusako aliyekua anakaimu kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa.
Manji amesema Beno Njovu anaanza kuitumikia hiyo nafasi mpya kuanzia leo na Mwalusako atakua naye pamoja kwa kipindi cha mwezi mmoja hadi atakapomkabidhi kazi rasmi.
Aidha, Manji amesema Mkutano Mkuu wa wanachama utafanyika Januari 19, mwakani na wanachama watapata fursa ya kupitia taarifa ya mapato na matumizi pamoja kujadili ajenda nyingine mbalimbali.
Pamoja na hayo, Kikao cha Kamati ya Utendaji kilichoketi mwishoni mwa wiki, kimemteua Seif Ahmed ‘Magari’ kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kimataifa na kutokana na nafasi hiyo pia ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Utendaji.
Jumatatu, 9 Desemba 2013
YAFAHAMU MAAJABU 10 YA HAYATI NELSON MANDELA.

RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela, mweusi wa kwanza kushika wadhifa huo katika taifa lenye uwezo mkubwa kiuchumi na
kijeshi barani Afrika, alifariki dunia Alhamisi iliyopita akiwa nyumbani kwake jijini Johannesburg.
Kifo chake kimeushtua ulimwengu na kwa mara ya kwanza katika historia, dunia nzima imesimama nyuma ya jemedari huyo, kila mmoja akionesha masikitiko yake.
Wakati dunia ikisubiri mazishi yake ambayo pia yatavunja rekodi ya mazishi yote yaliyowahi kufanywa tokea kuumbwa kwa uso wa dunia hapo Desemba 15 mwaka huu, Uwazi limebaini maajabu kumi yanayoambatana na msiba huo.
AIR FORCE ONE KUBEBA MARAIS WATANO WA MAREKANI.
AIR Force One ni ndege inayombeba Rais wa Marekani aliye madarakani na kumpeleka popote duniani. Lakini katika hali ya kushangaza, Idara ya Usalama ya Marekani imetoa ruhusa kwa marais wastaafu wakiwa na wake zao, kuandamana na Rais Barak Obama kuhudhuria mazishi ya shujaa huyo wa dunia.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo lenye nguvu kubwa duniani kuwapakia katika ndege hiyo yenye kila kitu ndani yake, marais wake kwa wakati mmoja.
Marais hao ni Obama mwenyewe na mkewe Michelle, George Bush na mkewe Laura, Bill Clinton na mkewe Hillary, Rais wa 39 wa Marekani, Jimmy Carter naye atakuwepo ila baba yake George W. Bush, George Bush senior huenda asiende kutokana na urefu wa safari hiyo.
QUNU; KIJIJI KITAKACHOLNDWA KULIKO VYOTE DUNIANI
Mandela alizaliwa katika Kijiji cha Qunu, kilichopo katika Jimbo la Eastern Cape, kilometa 32 Kusini Magharibi mwa mji wa Mthatha.
Kutokana na tukio hilo kubwa la mazishi, Jeshi la Afrika Kusini ambalo ni bora zaidi barani Afrika, limechukua jukumu la kusimamia ulinzi wote. Lakini uwepo wa Rais Obama na watangulizi wake wanne, utaifanya nchi hiyo kuchukua tahadhari zaidi ya kuhakikisha hakuna dosari yoyote ya kiusalama inayoweza kujitokeza.
Ulinzi huo umeimarishwa zaidi kutokana na ukweli kwamba viongozi wakubwa karibu wote wa dunia watahudhuria mazishi hayo, akiwemo Papa Francisco, Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon. Hakuna uwezekano wowote wa Al shaabab kusababisha rabsha kwani wameshadhibitiwa kwa ulinzi mkali.
MANDELA ALIKUWA ‘GAIDI’ PEKEE ALIYEGEUKA KUWA SHUJAA
Kwa miaka mingi, mataifa ya magharibi pamoja na Marekani walimchukulia Mandela na harakati zake kama gaidi. Wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, chama cha ANC kilikuwa na jeshi lake lililofahamika kama Umkhonto we Sizwe. Wazungu wa Magharibi na Marekani ambao walikuwa wakiwaunga mkono Makaburu, waliiona ANC kama kikundi cha kigaidi na hivyo Mandela naye akawekwa katika orodha ya magaidi duniani.
Hata hivyo, baada ya kutoka jela na kuchaguliwa kuwa Rais wa Afrika Kusini, Mandela aligeuka kuwa kipenzi cha watu hao ambao walilazimika kumuondoa katika orodha ya magaidi na leo hii akiwa amefariki dunia, anapewa heshima kubwa kuliko aliyowahi kupewa mzungu yeyote duniani.
MWEUSI PEKEE ALIYENYENYEKEWA NA WAZUNGU
Hayati Mandela ndiye mtu mweusi pekee duniani aliyewahi kupewa heshima zisizo na mfano tokea kuumbwa kwa dunia. Mara baada ya kutangazwa kwa kifo chake, viongozi wa mataifa yote makubwa duniani walionesha masikitiko yao na kila mmoja alimsifu kama mtu wa aina ya pekee kuwahi kuwepo chini ya jua (ukiachia mbali mitume na manabii).
JENGO LA SERIKALI NEW YORK LAPAKWA RANGI YA BENDERA YA SAUZI
Jengo moja la serikali jijini New York, Marekani limebadilishwa taa za kulipamba na kuonesha bendera ya taifa la Afrika Kusini.
WENYEJI WAHAMA, WAGENI WAMILIKI NYUMBA QUNU
Kijiji cha Qunu, sehemu ambayo yatafanyika mazishi ya Mandela, kuna eneo dogo kulingana na ugeni mkubwa unaotarajiwa kuwepo. Taarifa kutoka huko zinasema wenyeji, pamoja na machungu waliyonayo kutokana na kifo cha mzee huyo, pia watafaidika kiuchumi kutokana na wageni wengi kutaka kupata nyumba za kukaa wakati wakiendelea na maombolezo.
Wanaotafuta nyumba kijijini hapo ni pamoja na watu kutoka vyombo mbalimbali vya habari, mashirika ya kimataifa na wageni binafsi.
Inadaiwa kuwa wenyeji wanasogea katika vijiji vya jirani ili kupangisha nyumba zao kwa muda.
MECHI ZA LIGI KUU ENGLAND ZAANZA KWA SALA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Chama cha Soka cha England (FA) kiliamuru mechi zote za ligi kuu zilizochezwa wiki iliyopita, lazima zianze kwa sala maalum ya kumuenzi mzee Mandela.
Hii ni mara ya kwanza kwa agizo hilo kutolewa kwa heshima ya kiongozi mstaafu aliyefariki dunia asiye Mwingereza, tena akitokea barani Afrika. Tukio kama hilo pia limefanywa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ambalo limeamuru bendera yake iliyo katika mataifa yote wanachama duniani, ishushwe nusu mlingoti kwa heshima ya Tata Madiba!
NASA YATOA ZAWADI YA PICHA YA SAUZI KUTOKA ANGANI
Taasisi ya utafiti wa anga za juu nchini Marekani (NASA) kwa kutambua mchango mkubwa wa Mandela katika amani ya dunia, imetangaza kutoa zawadi kwa watu wa Afrika Kusini, itakayoonesha picha ya nchi hiyo inavyoonekana kutoka angani.
UINGEREZA YAAGIZA BALOZI ZOTE KUSHUSHA NUSU MLINGOTI
Serikali ya Uingereza imeziagiza balozi zote za kigeni zilizopo nchini humo kushusha bendera zao nusu mlingoti kama moja ya heshima na maombolezo ya kifo cha Mzee Nelson Mandela.
Hili ni agizo la aina yake kuwahi kutolewa kuhusiana na msiba wa kiongozi yeyote, kwani suala la kushusha bendera mara nyingi ni uamuzi wa serikali husika na si kwa shinikizo kama ilivyotokea Uingereza.
AMSAFIRISHA PAPA MAZISHINI
Historia ya utumishi wa kiongozi mkuu wa Madhehebu ya Romani, papa haioneshi kama aliwahi kuhudhuria mazishi ya rais au rais mstaafu, kitendo cha Papa Francisco kuhudhuria mazishi hayo kumeongeza ajabu katika mazishi ya Mandela, wengi wakisema hakina hakuwa mtu wa kawaida.
DIAMOND, CHEGGE NA MWASITI WALIVYONOGESHA USHINDI WA STARS DHIDI YA UGANDA CHALLENGE MOMBASA
DIAMOND, CHEGGE NA MWASITI WALIVYONOGESHA USHINDI WA STARS DHIDI YA UGANDA CHALLENGE MOMBASA
DIAMOND, CHEGGE NA MWASITI WALIVYONOGESHA USHINDI WA STARS DHIDI YA UGANDA CHALLENGE MOMBASA USIKU HUU
![]() |
| Chegge wa TMK naye akifanya vitu vyake Mombasa |
![]() |
| Mashabiki wa Tanzania walikuwepo ukumbini |
![]() |
| Queen Darleen akiimba |
![]() |
| Abdul Kiba alikuwepo pia |
![]() |
| Maunda Zorro naye |
![]() |
| Mwasiti pia |
![]() |
| Hata Peter Msechu |
![]() |
| Binti akiikakitikia kamba wakati Chegge anaimba |
MCHEKI DIAMOND NA NGASSA WAKIWA KWENYE NDEGE FULL BATA
DIAMOND NA NGASSA KWENYE PIPA...PLUTINUMZ AITAKIA KILA LA HERI STARS CHALLENGE
DIAMOND NA NGASSA KWENYE PIPA...PLUTINUMZ AITAKIA KILA LA HERI STARS CHALLENGE
Jumapili, 8 Desemba 2013
WEMA KAMISS PENZI LA DIAMOND?.TAZAMA PICHA ALIYOPOST NA MANENO ALIYOANDIKA.
WEMA KAMISS PENZI LA DIAMOND.TAZAMA PICHA ALIYOPOST NA MANENO ALIYOANDIKA.
Mcheza filamu za kibongo Wema Sepetu ametuma picha ya mpenzi wake wa zaman mwanamuziki Diamond Platnamu kwenye akaunti.yake ya instagram na kuandika,“ i jus happen to love dis picture“
baada ya kuweka picha hiyo mashabiki wameanza kumsifia uku wakimponda mpenzi Penny ambae anaaminika ndio mpenzi wa Diamond kwa sasa
Website hii imepitia akaunti ya Diamond na kukuta picha ile ile aliyoweka Wema ikiwa na maneno kuonesha kua usiku wa jana msanii huyu alikua kwenye sherehe ya kuzaliwa mrembo wa zamani wa Tanzania Jackline Ntuyabaliwe.
Alhamisi, 5 Desemba 2013
Breaking News,Nelson Mandela Amefariki Dunia
Habari kuhusu kifo cha Nelson Mandela zimetangazwa na Rais wa sasa wa Africa Kusini Bwana Jacob Zuma mida ya saa saba usiku kuamkia leo December 6 2013. Pia vyombo vya habari Bbc Na CNN vimetangaza kuwa Mandela amefariki akiwa na miaka 95 na alikuwa
hospitalini kwa muda mrefu akipata matibabu.
CNN Wana Repoti kuwa Mwezi wa tatu mwaka 2013 Mandela aliumwa sana na raia wangi Africa Kusini walijua watampoteza Mandela ila haikuwa hivyo na hali yake ikawa nzuri kwa muda na baadae kurudishwa hospitalini baada ya kuzidiwa.
Bendera zote Africa Kusini zimeanza kupepea nusu mlingoti baada ya kutangazwa kwa kifo cha Nelson Mandela.
BABY MADAHA ASEMA DIAMOND NI MZINZ!!! DIAMOND NAE AFUNGUKA KUMPONDA TIZAMA HAPA
ACHANA na mabifu yaliyotangulia, hili ni jipya kabisaa! Msanii wa sinema na Bongo Fleva, Baby
Joseph Madaha ameingia kwenye bifu zito na Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ na kudai staa huyo wa Wimbo wa Number One ni mzinzi ‘fuska’
Bila kumung’unya maneno, mapema wiki hii, Baby Madaha alimvaa Diamond ambaye ni Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB) akimtuhumu kuwa na tabia za kifuska.
Baby Madaha alidai hata muziki anaoufanya Diamond kamwe hauwezi kulingana na mafanikio makubwa ya jina lake zaidi ya kubebwa na skendo tu.
CHOKOCHOKO ZILIVYOANZA
Kupitia mitandao ya kijamii, ilivuja posti ambayo ilidaiwa kutoka kwa Baby Madaha ikimpaka Diamond kuwa siyo mwanamuziki kama ilivyo kwa wasanii wengine wenye uwezo mkubwa, akitolea mfano Elias Barnaba wa THT.
Sehemu ya posti hiyo ilionesha kuwa, Diamond si msanii wa muziki bali ni mzinzi f’lani hivi anayefanya biashara ya muziki kupitia mapenzi.
“Siku wanawake maarufu nchini Tanzania watakapojitambua na kuacha kulewa penzi la Diamond, huo ndiyo utakuwa mwisho wa maisha yake kimuziki kwa sababu hatakuwa na jipya na hivyo soko lake litaporomoka,” ilisomeka posti hiyo.
UKWELI NI UPI?
Baada ya ishu hiyo kugeuka habari ya mjini na kuibuka kwa makundi mawili yanayokinzana, Amani lilimtafuta Baby Madaha ili kujua ukweli wa posti hiyo ndipo akatiririka aya za kuthibitisha kuwa picha haziivi, hamkubali Diamond na kudai hata kimuziki hamkubali kwani anaamini wapo wanamuziki wanaofanya vema katika gemu kuliko yeye.
“…tuseme ukweli, Diamond ni mfanyabiashara siyo mwanamuziki. Kuhusu hiyo posti iwe ni mimi nimeandika au si mimi lakini kimsingi hayo maneno yanamstahili kabisa. Mzinzi tu.
“Diamond anabebwa na media (vyombo vya habari). Kuna wanamuziki wengi wazuri sembuse yeye? Ana nini haswa?” alihoji Baby.
AMANI LAMGEUKIA DIAMOND
Baada ya kusikia maelezo ya Baby kwa kifupi, Amani lilimuweka ‘pending’ kwa muda na kumwendea hewani Diamond ili liweze kujua upande wake analizungumziaje bifu hilo ambalo lilikuwa likienea mitandaoni kama moto wa kifuu.
Tofauti na matarajio ya mapaparazi wetu kwamba huenda angejibu mashambulizi makali kwa Madaha, Diamond au ‘Sukari ya Warembo’ aling’aka huku akimponda mwanadada huyo na kumshangaa:
DIAMOND SASA
“Daaah! Huko ni kunishusha…mimi na huyo (Baby) wapi kwa wapi kamwe huwezi kunilinganisha na mtu ambaye yupo chini yangu sana, nikijibizana naye nitajishusha tu. Ingekuwa ni mtu mkubwa mwenye levo yangu hapo ningesema natakiwa kusema neno.
“Hana lolote huyo anatafuta ‘kiki’ tu kupitia mimi, nipo na dili zangu za maana nipoteze muda kwake? Atafute wa levo yake na wala si mimi.”
UZINZI VIPI?
Alipoulizwa kuhusu suala la uzinzi ambalo Baby Madaha aliumaanisha katika posti yake, Diamond aliendelea kukazia kuwa hana muda wa kupoteza kwa mtu kama Baby Madaha ambaye kimsingi ni kama ardhi na mbingu.
“Huyo anatafuta kiki tu, aachane na mimi…mbona hatufanani kabisa mimi na yeye wapi kwa wapi?” alikazia Diamond a.k.a Weka Mbali na Watoto Wazuri wa Kike.
BABY AREJEA HEWANI
Wakati mapaparazi wetu wakimalizana na Diamond, kilongalonga kimoja cha paparazi wetu kilikuwa kikionesha kinaita, ilivyokatika ya Diamond, Baby akapanda hewani kwa mara nyingine.
Safari hii alimchana laivu: “Nimeisoma upya posti yenyewe, kilichopo humu ni ukweli mtupu. Hakuna hata tone la uongo, wewe utamlinganisha Diamond na mtu kama Barnaba? Huyu ni mfanyabiashara tu, hajui kuimba kwa kutumia vyombo kama mimi.
“Diamond hawezi kupiga chombo hata kimoja cha muziki atajiitaje mwanamuziki? Anastahili kabisa ujumbe huu.”
UFUSKA
Mapaparazi wetu walilazimika kumtwanga swali Baby Madaha kuhusiana na ufuska ambao ulikuwa umetajwa katika maelezo ya awali, kama endapo Diamond ni mzinzi au yeye ndiyo mzinzi.
Katika maelezo yake, Baby Madaha aliwashangaza mapaparazi wetu kwa kutaja namna gani anaweza kumuita Diamond mzinzi. Sikia:
Amani: “Umesema Diamond si mwanamuziki, je, suala la uzinzi ni nani analo kati yako na yeye?”
Baby: “Mimi si mzinzi. Diamond ndiyo mzinzi tena sana tu.”
Amani: “Uzinzi wake upo wapi?”
Baby: “Kitendo cha kubadilisha wanawake, kufumaniwa na Wema Sepetu akiwa na Jokate Mwegelo ndiyo uzinzi wenyewe huo.”
Amani: “Kwani wewe hujawahi kuwa na wanaume tofauti? Hujawahi kufumaniwa?”
Baby: “Mimi sijawahi, yeye amewahi na hakuwahi kukanusha hivyo inadhihirisha kuwa ni kweli. Kwangu mimi kila aliyetajwa kutoka na mimi kama haikuwa kweli, nilikanusha mara moja yeye mbona hakanushi?”
Amani: “Kwani Diamond alifumaniwa na nani?”
Baby: “Acha hizo, kwani hukumbuki kipindi cha Wema? Mara alinaswa na Aunt mara na… yule ndiyo mzinzi sasa.”
KWANI WALITONGOZANA?
Kuhusu suala la kutongozwa, Baby alisema Diamond hajawahi. Cha kushangaza zaidi, alisema hata kama ikitokea siku staa huyo akamtongoza kamwe hawezi kumkubalia kwani hawaendani hata kidogo.
Alisema yeye ni mtu wa kutembea na vigogo na si vitoto kama Diamond.
“Hana hela, kamwe siwezi kumkubalia. Ni mtu ambaye ana vihela mbuzi sasa mtu kama yeye mimi wa nini? Ndiyo maana aliwahi kukimbiwa na mwanamke kwa kuwa hana hela.
“Tena yule mwanamke akaenda kwa kigogo mwenye hela, mimi na yeye ni mbalimbali kabisa. Hata muziki ninaofanya hauwezi, mimi ninaimba RnB yeye anafanya Pop, tuko tofauti kabisa,” alisema Baby pasipo kumtaja mwanamke aliyemkimbia Diamond.
TUJIKUMBUSHE PANDE ZOTE
Diamond aliwahi kuripotiwa kutoka kimapenzi na ‘totoz’ kibao wakiwemo yule wa mwanzo aliyemzingua aitwaye Sarah, Rehema Fabian, Jacqueline Wolper, Upendo Mushi ‘Pendo wa Maisha Plus’, Wema Sepetu, Natasha (Video Queen wa Wimbo wa Moyo Wangu), Najma (aliwahi kuwa mpenzi wa Mr. Blue), Jokate Mwegelo, yule demu wa Kenya na aliyekuwa mwigizaji aliyefulia ambaye ni mke wa mtu.
Kwa upande wake Baby Madaha anayekimbiza na ngoma yake ya Summer Holiday
Jumatano, 4 Desemba 2013
| Arsenal - Hull City | 2 - 0 | |
| Liverpool - Norwich | 5 - 1 | |
| Man. United - Everton | 0 - 1 | |
| Southampton FC - Aston Villa | 2 - 3 | |
| Stoke City - Cardiff | 0 - 0 | |
| Sunderland - Chelsea | 3 - 4 | |
| Swansea - Newcastle Utd | 3 - 0 | |
| Fulham - Tottenham | 1 - 2 | |
| West Bromwich - Man. City | 2 - 3 |
| haya ni matokeo ya
mechi za jana usiku poleni mashabiki wa Manchester united |
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)





































.jpg)



