Tafuta katika Blogu Hii

Alhamisi, 15 Januari 2015

Mawindo ya usajili barani ulaya chelsea,man yajue hapa...............


Bossi wa Manchester City Manuel Pellegrini amefungua milango ya kutaka kumsajili mshambuliaji Lionel Messi toka Barcelona, ambapo wako tayari kuvunja benki kwa kutoa kitita cha £480milioni.
Arsenal wako tayari kutoa £63milion kwa klabu Borussia Dortmund ilikuweza kuwasajili nyota wawili wa timu hiyo kiungo Ilkay Gundogan na beki Mats Hummels.
Timu ya Palermo imekataa kukubali ofa ya kuumza mshambulaiji wake Paulo Dybala,kwa Manchester United mchezaji huyu anakadiriwa kuwa na thamani ya £30milioni.
Paris St-Germain, Porto na Juventus wanapigana vikumbo katika kutaka kumsajili kwa mkopo kinda Adnan Januzaj mwenye miaka 19 toka Manchester United.
Crystal Palace wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji Bafetimbi Gomis, toka Swansea City kwa ada ya uhamisho ya £8milion.
Meneja wa West Brom Tony Pulis anataka kumsajili kiungo mkongwe wa Manchester United Darren Fletcher mwenye miaka 31, ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chake.

Swansea wanataka kutumia pesa walizopata kwa kuuza mshambuliaji Wilfried Bony kumsajili kiungo Alexandru Maxim toka Stuttgart ya Ujerumani
Manchester United wameanza mazungumzo na klabu ya PSG ili dau £30milion ili kumnasa la kumsajili mlinzi Marquinhos raia wa Brazil.
Kocha Jose Mourinho yuko tayari kuwatoa Andre Schurrle, na winga Mohamed Salah,il;I kupata pesa ya kumnunua beki Raphael Varane wa klabu ya Real Madrid.
Mshambauliaji wa Everton Kevin Mirallas amesema ataamua hatima mwishoni mwa msimu kama ataendelea kusalia Goodison Park au atahamia klabu nyingine

USHER RYMOND musician amvisha pete meneja wake wa zamani GRACE MIGUEL...............



Muimbaji huyo wa R&B ameamua kumchumbia girlfriend wake huyo pia meneja wake GRACE MIGUEL ambae USher amepitwa miaka nane na huyo mpenzi wake.

katika interview na gazeti la billboard october  2014.  usher alisema i have an incredible partner and meneja, amenisaidia katika kipindi kigumu nilicho pitia katika maisha yangu, ameka mtu anae ni support na muelewa kwangu.

Usher ni baba wa watoto wa kiume wawili aliwapata kipind yuko na mke wake wa zaman aliechana nae TAMEKA FOSTER.


MALKIA ELIZABETH ATOA TUZO KWA VIJANA WAWILI TANZANIA............






queen

MALKIA WA UINGEREZA anatarajia kutoa tuzo hiyo ijulikanayo kama 
‘The Queen’s Young Leader Award’

NI kwa vijana wawili ambao ni GIVEN EDWARD NA ANGELA MNAGOZAunnamed

Given Edward

Given realised that gridlock on the roads was cutting into valuable lesson time for students. So he created MyElimu.com, an online discussion forum where commuting pupils can continue discussing subjects. More than 500 students have registered so far and Given wants to carry on making education accessible for as many young people as possible in his country

 xxxxxxxxxxxxx


Angela Benedicto Mnagoza

Following the death of her mother and her aunt, Angela worked in domestic service where she was abused and exploited by her employer. She now promotes the rights of child domestic workers, educating this marginalised workforce and attempting to change attitudes towards them
 xxxxxxxxxxxxxxx




Diamond dancer Moze Yogo na Aunt Ezekiel in love??????...............




Aunty Ezekiel na Moses Iyobo waweka wazi penzi lao sasa


Staa wa Bongo Movie,Aunty Ezekiel amedhihirisha penzi lake na dansa wa msanii Diamond Platinumz,Mose Iyobo baada ya picha yao wakiwa wamekaa kimahaba iliyosambaa mtandaoni

Mara kadhaa msanii huyo wa Bongo Movie amekuwa akikana kuwa hana uhusiano na dansa huyo na kutoweka wazi mhusika wa ujauzito wake hivyo picha hiyo imeonyesha kuwa Mose Iyobo kuwa ni mhusika wa ujauzito huo.

ZARI ALALA KWA MAMA DIAMOND SIKIA HII ...........

Mrembo wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’.
Stori: Mwandishi Wa/ Amani
IMEFICHUKA! Mrembo wa Uganda ambaye kwa sasa ndiye ‘usingizi’ wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ hivi karibuni alitua Bongo na kulala nyumbani kwa mama wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’, Sinza-Mori jijini Dar.
Chanzo makini kilicho karibu na familia ya Diamond kimepenyeza ‘ubuyu’ kuwa, Zari alipata fursa ya kupiga ‘mbonji’ nyumbani hapo alipomtembelea Diamond.
“Alikuja akambonji kwa mama Diamond kama siku mbili hivi halafu wakaondoka wote wakati Diamond alipokwenda Nigeria kwenye shoo ya Mwanasoka Bora wa Afrika 2014.
“Awali, Diamond alitaka akamlaze hotelini lakini mtoto wa kike akakataa, akasema anataka kuangusha usingizi nyumbani kwa mkwewe, Diamond akasema ruksa mama,” kilisema chanzo hicho.
Kikizidi kumwaga data, chanzo kilisema, mbali na kulala, Zari alishiriki kazi za ndani ikiwemo kupika na kupakua kama ilivyokuwa kwa zilipendwa wa Diamond, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Wema Sepetu.
Alipoulizwa Diamond kuhusiana na suala hilo hakutaka kufafanua mengi zaidi ya kukiri kwamba mrembo huyo alikuja Dar na kuondoka naye.
Zarinah Hassan ‘Zari’ akiwa na 'Diamond Platnumz'.
“Wewe jua alikuja, nikaondoka naye hayo mambo mengine siwezi kuyazungumzia,” alisema Diamond.
Amani lilipomtafuta mama Diamond kwa njia ya simu hakupatikana lakini mtu wa karibu alisema kwa sasa hatumii simu kwa sababu ambazo hazikutajwa

Jumatano, 14 Januari 2015

MAMBO YA USAJILI ULAYA HAYA HAPA ..........



Hatimaye Manchester city wamekubali kutoa kitita cha pauni million 27 kwaajilia ya kumnuna mchezaji wa Swansea city na timu ya taifa ya ivory coast ambae amepewa mkataba wa miaka minne na nusu kwaajili ya kuisaidia timu ya Manchester city kuchukua ubingwa wa ligi.
Tayari Bony n mchezaji wa man city huu uhamisho unamfdanya bony kuweka history yakuwa mchezji ghali wa Africa ambae analipwa mshahara wa pauni 115,000 kwa week.
City watamsubiri bony mpaka atakapo rudi kutoka kombe la mataifa ya afrika  pamoja na mchezaji tegemeo wa Manchester city yaya toure, lakin wakiwa na imani kuwa bony atafanya makubwa akiwa na timu hiyo ya Manchester
Bony inatakiwa aonyeshe uwezo alouonyesha mwaka 2014 kwa kuwa mfungaji mwenye magoli mengi akifuatiwa na kun Aguero akimaliza mwaka kwa magoli 20.

HIZI NI MALI ZA ZARI ZE BOSS BABY WA DIAMOND mjue kiundani.........

JINA la Zari hivi sasa limekuwa jina maarufu katika masikio ya Watanzania, Afrika Mashariki na kwingineko hasa baada ya mwanadada huyo mfanyabiashara na mwanamuziki wa Uganda kuwa na urafiki na Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassib Abdul maarufu kwa jina la usanii Diamond Platnum.

Zari The Lady Boss
Kwenye mitandao ya kijamii kama Tweeter, Facebook,Instagram na hata Whatsapp lazima utakutana na jina Zari akiunganishwa na Diamond na wengine wataunganisha na Wema Sepetu aliyewahi kuwa mpenzi wa Diamond.

Uhusiano kati ya Zari na Diamond umezua gumzo kila eneo Tanzania na Afrika Mashariki huku wakifananishwa na mastaa wa nje kama vile Kanye West na Kim Kardashian kwa namna wanavyofuatana wakati wote huku Diamond akionesha kila aina ya mbwembwe za kumjali mrembo huyo kutoka Kampala, Uganda.

Uhusiano wa Zari na Diamond umewafanya kuandamana kila sehemu hivi sasa. Wawili hao walianza kuonekana kuwa na ukaribu wa mahusiano tangu Diamond alipokwenda Afrika Kusini kwenye Tuzo za Channel O ambapo Diamond aliibuka na ushindi wa Tuzo tatu.

Baada ya Tuzo hizo, Zari alimualika Diamond kushiriki katika ‘pati’ maarufu ambayo mwanadada huyo huandaa kila mwaka nchini Uganda ambapo mwaka huu ilijulikana kama All White Ciroc Party.

Wawili hao baada ya sherehe hiyo, walifuatana ambapo Zari alimsindikiza Diamond nchini Rwanda na Burundi alipokwenda kutoa burudani nchini humo, na picha kusambazwa katika mitandao ya kijamii na kuwafanya wawili hao kuwa gumzo hivi sasa katika mitandao Tanzania na Afrika Mashariki.

Je, Zari ni nani hasa? Zarina Hassan Tlale.Maarufu kama Zari ni Mganda anayeishi Afrika Kusini.

Mrembo huyo ni mwanamuziki na mfanyabiashara. Ni mwanamke aliyefanikiwa na anayependa kuishi maisha ya kifahari. Anamiliki magari ya kifahari na yenye gharama kubwa kama Lamborghini Gallardo, BMW- 2006,Chrysler-2008, Audi Q7-2010 na Ranger Rover Sports .

Mwanadada huyo ni binti wa Halima Sultan Hassan na Nasur Hassan akiwa na asili ya damu mchanganyiko ikiwa ni pamoja na ya Kihindi , Toro, Somalia na Burundi kutoka mji wa Jinja, Uganda. Babu mzaa mama yake anatoka India na bibi yake ni kutoka Uganda. Babu yake mzaa baba ni kutoka Somalia na bibi yake mzaa baba anatoka Burundi.

Zari maarufu kama The Bosslady aliwahi kuolewa na mwanamume anayejulikana kwa jina la Ivan na kubarikiwa watoto watatu wa kiume Pinto, Didy na Quincy na anamiliki kampuni tatu.

Mwanadada huyu alizaliwa Septemba 23,1980. Zari amekulia katika mji wa Jinja katika nchi ya Afrika Mashariki inayojulikana kama Uganda.

Zari alisoma shule ya msingi, kisha kwenda Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jinja ambapo alisoma kwa bidii kutimiza ndoto zake. Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, mwanadada huyo alihamia katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala ambapo alikuwa akitoa burudani ya muziki katika maeneo ya starehe kabla ya kuhamia mjini London, Uingereza na kusomea Stashahada ya masuala ya urembo (cosmetology).

Historia yake kimuziki inaonesha Zari alianza kuimba akiwa na umri mdogo wakati akisoma shule ya msingi ambapo alikuwa akitoa burudani katika matamasha ya muziki yaliyokuwa yanaandaliwa na wafanyakazi wa shule,wakati wa hafla za mwishoni mwa mwaka na katika mashindano mengine ya jumuiya akiwakilisha shule yake.

Ingawa amekulia katika familia ya Kiislamu yenye wasichana sita na wavulana wawili, Zari hakuacha mapenzi yake kwenye muziki. Alianza muziki akiwa na umri mdogo na albamu yake ina nyimbo kali kama ‘Toloba’ na ‘Hotter Than Them’. Watu waliomvutia katika muziki ni Wasanii wa Marekani Arethal Franklin na Whitney Houston wakati akiwa sekondari.

Afrika waliomvutia akapenda muziki ni wanamuziki wa Afrika Kusini Brenda Fassie, Miriam Makeba, Lucky Dube na Malkia wa Muziki Afrika Kusini, Yvone Chaka Chaka. Alipojiunga na sekondari alijiunga na makundi ya dansi,drama na muziki jambo ambalo lilimsaidia kuchaguliwa kwa miaka miwili mfululizo la Muigizaji Bora.

Baada ya miaka miwili ya kufanya vizuri katika majukwaa na matamasha ya shule, alipumzika na kuhama kutoka Uganda kwenda London, Uingereza na kuendelea na masomo yake lakini bado mapenzi yake kwa muziki yakiwa mawazoni mwake. Zari kwa msaada wa familia, mashabiki na marafiki wa- naopenda mtindo wa muziki wake na kuamini anaweza aliamua kuchukua hatua mwaka 2007 wa kurekodi singo yake ya kwanza inayoitwa Oliwange (ikiwa na maana wewe ni wangu) .

Mwaka 2008 Zari alishinda Tuzo ya Channel O ya Video Bora ya Muziki ya Msanii Bora Afrika Mshariki. Hafla ya tuzo hizo ilifanyika Johannesburg, Afrika Kusini. Tangu hapo Zari ameendelea kutoa nyimbo zaidi za kuvutia, huku akitiwa moyo na mashabiki wake wakati huo.

Mwaka 2009 alipata Tuzo inayojulikana kama Diva ya mwaka katika kipengele cha Diaspora tangu hapo aliendelea kutengeneza muziki. Zari hivi sasa anaishi Afrika Kusini ambapo anamiliki maduka makubwa ya vipodozi na shule ya elimu ya juu mjini Pretoria wakati akiendelea kujijenga kimuziki.

Inaelezwa kuwa Zari na aliyekuwa mumewe Ivan wanamiliki Shule ya Brooklyn City ambayo ina kampasi sita Afrika Kusini, huku kila moja ikiwa na wanafunzi kati ya 800 hadi 2,100. Wanafunzi hao hupewa vyeti vya taifa wanapomaliza mwaka. Vile vile Zari amejenga hosteli iliyopo barabara ya Sir Apollo Kaggwa, Kampala na anamiliki nyumba kadhaa katika mji huo hasa eneo la Munyonyo, pamoja na duka kubwa la nguo Afrika Kusini.

Ingawa muziki wake haujafanya vizuri kama wanamuziki wengine wa Uganda akiwemo Jose Chameleone, Bebe Cool, Bobi Wine na Ragga Dee, Zari amekuwa akifurahia kwa mafanikio zaidi kwenye biashara na kutokana na hilo anasema lazima arudishe kwa jamii na hivyo kuamua kusaidia vituo na taasisi kadhaa zinazohitaji misaada kama Katalemwa Cheshire Home, Sanyu Babies’ Home pamoja na Gereza la Luzira.

Mfano mwaka 2013 kutokana na moyo wake wa kusaidia,kwa kutimiza hilo baada ya sherehe zake anazozifanya kila mwisho wa mwaka aliamua kutembelea Kituo cha Watoto Yatima cha M-Lisada kilichopo Nsambya siku moja kabla ya Sikukuu ya Krismasi, akifuatana na watoto wake Pinto, Didy na Quincy.

Alitoa zawadi maalum kwa watoto hao, ambapo Zari alishiriki kuandaa chakula cha Krismasi na kisha baadaye wanawake, sukari, biskuti, mchele na matoke. Mbali na masuala mengine yote, kwa mujibu wa tafiti mbalimbali,watu wengi nchini Uganda wanakubaliana kuwa Zari ndio Mwanamke Mrembo zaidi nchini humo.

“Sitafuti umaarufu, wenyewe umaarufu ndio hunifuata,”aliwahi Zari kusema kupitia mtandao wa Red Pepper akikanusha habari za baadhi ya watu wanaodai kuwa anatafuta umaarufu kwa nguvu.

Habari zake kuandikwa katika mitandao ya kijamii pamoja na shughuli zake za uhisani zimesababisha wengi kudai kuwa anataka tu umaarufu, kujulikana na kuzungumziwa kila wakati.Hata hivyo akijibu madai hayo, Zari alisema umaarufu unamtafuta yeye na sio kwamba yeye anautafuta.